Blinken anatarajiwa kukutana na Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Rais wa Palestina Mahmud Abbas huko Ramallah. / Picha: Reuters
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema Alhamisi kwenye ziara yake nchini Israel kwamba, makubaliano ya muda ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas yalikuwa "yameleta matokeo" na yanapaswa kuendelea.

Kama sehemu ya kusitisha mapigano, iliyoko katika siku yake ya saba, Hamas imewaachilia mateka kadhaa waliochukuliwa wakati wa shambulio lake mnamo Oktoba 7 kwa minajili ya kuachiliwa kwa zaidi ya wafungwa 200 wa Palestina wanaoshikiliwa katika magereza ya Israeli.

"Tumeona, wiki iliyopita, maendeleo mazuri sana ya mateka kurudi nyumbani, kuungana tena na familia zao," Blinken alisema katika mkutano na Rais wa Israeli Isaac Herzog huko Tel Aviv.

Blinken, anayezuru eneo hilo kwa mara ya tatu tangu vita kuanza, pia anatarajiwa kukutana na Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Rais wa Palestina Mahmud Abbas huko Ramallah.

"Pia imewezesha ongezeko la misaada ya kibinadamu kwenda kwa raia wasio na hatia huko Gaza ambao wanahitaji sana.

"Kwa hivyo mchakato huu unatoa matokeo. Ni muhimu, na tunatumai kuwa inaweza kuendelea."

Blinken, aliyezuru eneo hilo kwa mara ya tatu tangu vita kuanza, pia anatarajiwa kukutana na Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Rais wa Palestina Mahmud Abbas huko Ramallah.

AFP