Idadi ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina waliokamatwa wakati wa maandamano katika Chuo Kikuu cha Texas imeongezeka nakufika watu 34, mamlaka ilisema.
"Kufikia saa 9 alasiri, watu 34 wamekamatwa na vyombo vya sheria kwenye chuo kikuu cha UT Austin katika maandamano ya leo," Idara ya Usalama wa Raia ya Texas ilisema kwenye mtandao wa "X".
Miongoni mwa waliokamatwa ni mpiga picha wa FOX 7 Austin ambaye alikuwa akirekodi maandamano ya wanafunzi katika chuo cha UT Austin.
Picha kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha mpiga picha huyo akisukumwa chini na kufungwa pingu.
Wanafunzi hao waliandamana kukitaka chuo kikuu kuachana na ushirikiano na Israeli.
Maandamano hayo yaligeuka kuwa vurugu baada ya askari wa Idara ya Usalama wa Umma wa Texas kuingilia kati.
Maandamano hayo ni sehemu ya maandamano yanayofanyinka nchi nzima kuunga mkono Palestina, ambayo yanatoa wito wa taasisi za elimu kuachana na kampuni zinazofanya biashara na Israeli.
Idara ya Usalama wa Raia ilisema inatii amri ya chuo kikuu na Gavana Greg Abbott.
Abbott alisema kukamatwa kwa waandamanaji kutaendelea hadi pale maandamano yatakapomalizika.