Benki ya Dunia imeongeza kwa kiasi kikubwa azma yake ya kuunganishia Waafrika umeme ifikapo mwaka 2030, kutoka milioni 100 hadi zaidi ya milioni 250, Rais wa Benki hiyo alisema Jumatano.
Kulingana na Taasisi hiyo ya Kimataifa ya Fedha, watu milioni 600 barani Afrika wanakosa huduma muhimu ya umeme wa bei nafuu na wa kutegemewa - jambo ambalo linalokwamisha uundaji wa nafasi za kazi na maendeleo ya kiuchumi katika bara la Afrika.
"Huko nyuma katika mkutano wa COP28, Benki ya Dunia ilitoa ahadi ya kuunganisha Waafrika milioni 100 nishati ya bei nafuu ifikapo mwaka 2030," Rais wa Benki ya Dunia Ajay Banga alisema katika makao makuu ya Benki hiyo mjini Washington.
"Tutazidisha idadi hiyo ifikie watu milioni 250 kati ya watu milioni 600," aliongeza.
Lengo la ufadhili
Ili kuunganisha watu wengi kwenye gridi ya umeme ifikapo 2030, dola bilioni 30 za uwekezaji wa sekta ya umma zitahitajika, Benki ya Dunia ilisema katika taarifa.
Benki ilijitolea kutenga dola bilioni 5 kwa mradi huo mwaka jana, kiwango hicho kikipungua dola bilioni 25 kufikia malengo ya hapo awali.
Benki hiyo inategemea kukusanya na kutenga dola bilioni 15 zaidi kupitia njia yake wa kukopesha kwa masharti nafuu, Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA), na kuacha dola bilioni 10 za ziada kutolewa kutoka kwa "fedha za umma," msemaji aliiambia AFP.
"Watu milioni 600 katika bara hawana umeme," Banga alisema. "Kwangu mimi, hiyo ni hali isiyokubalika haswa katika mwaka wa 2024."
Lengo kuu
“Kupelekea wananchi umeme ni lengo la kwanza, pili na la tatu,” alisema.
Kando na Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika inatazamia kuunganisha watu wengine milioni 50 kwenye gridi ya stima kote barani Afrika, ifikapo mwisho wa muongo huu, Banga alisema.
"Ikiwa tunaweza kufikia 300 kati ya 600 ifikapo 2030, itakua ni jambo zuri," aliendelea.
"Hiyo ndiyo aina ya ahadi tunayohitaji kufanya," aliongeza. "Lakini hiyo itachukua juhudi kutoka sehemu zote za Benki."