Tanzania imesitisha uanzishaji wa bei elekezi za mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) zilizokuwa zikitarajiwa kuanza Januari 1, 2024.
Uamuzi huo unafuatia ukosoaji unaoongezeka na tishio linalowezekana la kususia kutoka hospitali kibinafsi.
NHIF ilikuwa imetangaza marekebisho ya kifurushi cha manufaa kinachoangazia bei za soko kwa huduma mahususi mnamo Disemba 18.
Lakini mabadiliko hayo yalichochea kutoridhika miongoni mwa wataalamu wa matibabu na vituo vya afya vya kibinafsi ambavyo walihisi kutengwa katika mchakato wa mashauriano, huku mamlaka za hospitali kibinafsi zikidokeza kuwanyima huduma wenye kadi za NHIF.
Huduma zilizochelewa
Hoja kuu ya mzozo ilikuwa mapendekezo ya kupunguzwa kwa ada za usajili na mashauriano.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitangaza kusimamisha kwa muda utekelezaji wa mpango huo mpya kufuatia mazungumzo na Jumuiya ya Vituo vya Afya Binafsi Tanzania, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC).
"Tunapongeza utulivu ulioonyeshwa na watoa huduma katika kipindi hiki," ilisema taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Wizara kwa Chama cha Watoa Hudua z Afya Binafsi-APHFTA na wadau wengine.