Rais wa Eritria akutana na wenzake kutoka Misri na Somalia jijini Asmara, Eritrea.

Mkutano wa kilelele wa siku mbili uliofanyika huko Asmara, Eritrea, ulioandaliwa na Rais Isaias Afwerki na kuhudhuriwa na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi, na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud umemalizika, baada ya viongozi hao watatu kutoa wito wa kuheshimiwa uhuru na uadilifu wa eneo la nchi katika eneo hilo.

Viongozi hao walishiriki katika mashauriano ya kina huko Asmara, yakilenga kuimarisha ushirikiano wao na kushughulikia kile walichokiita kama changamoto.

Katika taarifa iliyoonekana na TRT Afrika, lengo kuu la majadiliano ya viongozi watatu lilijikita katika kuhakikisha amani na usalama katika kanda hiyo walipokuwa wakithibitisha dhamira yao ya kuimarisha Jeshi la Taifa la Somalia ili kulinda mipaka ya ardhi na bahari ya Somalia na kusaidia kulinda uhuru na uadilifu wa eneo la nchi.

Katika mkutano huo muhimu, viongozi wa mataifa matatu walisisitiza umuhimu wa kuzingatia kanuni za msingi za sheria za kimataifa, wakiona kuwa ni vipengele muhimu kwa ajili ya kuimarisha utulivu wa kikanda na kuimarisha ushirikiano.

Walisisitiza hasa umuhimu wa kuheshimu uhuru na uadilifu wa eneo la nchi, katika eneo hilo, wakisisitiza kwamba misingi yoyote wa kuingilia katika masuala ya ndani unapaswa kukataliwa vikali.

Viongozi hao pia waliahidi msaada wao wa kimkakati ili kuchangia katika utulivu na usalama wa kikanda na kuimarisha uwezo wa Somalia kupambana na ugaidi na kushughulikia changamoto zinazohusiana nazo.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Eritrea na Somalia katika mkutano uliofanyika jijini Asmara, Eritrea, Alhamisi 10, Oktoba 2024.

Viongozi wa Eritrea, Misri na Somalia walitangaza zaidi kuanzishwa kwa kamati ya pamoja ya nchi tatu ili kusimamia na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa kidiplomasia katika sekta mbalimbali na kuongozwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Eritrea, Misri na Somalia.

Viongozi wa Somalia, Misra na Eritrea walipongeza pendekezo la Misri la kuchangia kutuma vikosi vyake Somalia katika juhudi za kulinda amani nchini humo.

TRT Afrika