Sehemu ya Uwanja wa Ndege wa Nairobi  JKIA, kufungwa kwa muda

Sehemu ya Uwanja wa Ndege wa Nairobi  JKIA, kufungwa kwa muda

Notisi hiyo inaonyesha kuwa kufungwa kwa sehemu ya uwanja kunafuatia ukarabati utakaoanza.
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya imesema upande mmoja wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta utafungwa kwa muda/ Picha: Wengine 

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Kenya yaani Kenya Airport Authority, KAA imewafahamisha abiria kwamba Terminal 1E katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta itafungwa kwa muda kuanzia Alhamisi, Oktoba 10.

Kituo cha 1E kinatumika kwa wanaowasili kimataifa.

"Katika kipindi hiki, mashirika yote ya ndege yaliyoathiriwa yatapitia Terminal 1A. Uamuzi huu umefanywa ili kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wetu na abiria wakati wa mchakato wa ukarabati,” KAA ilisema.

Notisi hiyo inaonyesha kuwa kufungwa kutaanzia saa moja asubuhi ili kuwezesha kazi muhimu za ukarabati.

"Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote ambao unaweza kusababisha na kuthamini uelewa wako na ushirikiano wakati huu," imesema ilani iliyotumwa na Kitengo cha Mawasiliano cha Shirika hilo.

TRT Afrika