Serikali ya Rwanda imetoa ilani kuhusu vidonge vya dawa vilivyotengezwa Kenya.
Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda, RFD, imeamuru kutolewa katika soko dawa za Fluconazole 200mg zilivyotengezwa na kampuni ya Universal Corporation Ltd, Kikuyu, Kenya.
Fluconazole hutumiwa kutibu maambukizi makubwa ya fangasi au chachu, pamoja na candidiasis ya uke, candidiasis, maambukizi mengine ya candida (pamoja na maambukizo ya njia ya mkojo, peritonitis [kuvimba kwa utando wa tumbo na mengine.
Shirika hilo la Rwanda lilielezea kampuni ya Universal Corporation Ltd, kuwa limegundua kubadilika kwa rangi katika vidonge vya Fluconazole 200mg, licha ya tarehe yake ya kuharibika kuwa mwaka 2025.
Dawa hiyo inapaswa kuwa na rangi ya pinki kabla ya kuharibika lakini ilikuwa imeanza kuonyesha rangi nyeupe tayari, kulingana na maelezo ya uchunguzi.
"Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda inawaagiza waangizaji wote wa dawa, wauzaji wa jumla wa matawi ya RMS, wauzaji wa reja reja, kibinafsi na wa umma kuacha usambazaji dawa zilizotajwa na kuzirudisha kwa msambazaji wao kwa usimamizi mzuri," taarifa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Rwanda imesema.
RFDA pia imesema kuwa waangizaji na wasambazaji wa dawa zilizotajwa hapo juu wana hadi siku 10 (tangu tarehe ya kutangazwa) kuripoti kiasi hiki kilichoagizwa, kusambazwa, kurudishwa na hisa ya mwisho mkononi.