Rais wa DRC Felix Tshisekedi akutana na viongozi wa Kivu Kusini na Kivu Kaskazini kujadili hali ya usalama Mashariki mwa DRC/ Picha: Ikulu DRC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Felix Tshisekedi amekutana na viongozi wa Kivu Kaskazini na kivu Kusini kuhusu hali ya usalama na matatizo kwa raia katika mji wa Goma uliovamiwa na jeshi la Rwanda.

" Hali katika jiji la Goma ni ya kusikitisha. Maiti zimeena kila sehemu, hakuna maji wala umeme kwa siku kadhaa, na wakazi hawana njia ya kupata chakula, " Ikulu ya DRC imemnukuu Safari Nganizi Jacques, Rais wa kikao cha viongozi waliochaguliwa wa Kivu Kaskazini.

“Kiongozi wa nchi alituhakikishia kuwa mchakato wa kidiplomasia unaendelea vizuri sana, anatarajia kuwa Jumuiya ya kimataifa itasikia sauti ya DRC na kuitaka Rwanda kuondoa wanajeshi wake, pia alituhakikishia kuwa anafanya kazi na MONUSCO na mashirika ya misaada kusaidia ndugu zetu, "alisema Nganizi.

Kwa sasa waasi wa M23 wametangaza kuudhibiti mji wa Goma Mashariki mwa DRC na wanadai kuwa sasa wanaelekea katika eneo la Kivu Kusini.

TRT Afrika