Dagalo alisisitiza kwamba anataka kurejea kwa amani kufuatia zaidi ya siku 100 za mapigano/ Picha: AFP

Mkuu wa Kikosi cha Msaada wa Haraka cha Kijeshi cha Sudan amewataka wapinzani wake katika afisa ya kitaifa ya jeshi kujiuzulu ili kuruhusu mapigano ya zaidi ya miezi mitatu kumalizika.

Katika video ya dakika tano inayoaminika kuwa ya kwanza tangu mapigano yalipozuka Aprili 15, Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo aliwaambia wanajeshi wa kawaida wa jeshi kwamba amani inaweza kurejeshwa "ndani ya masaa 72" ikiwa watamsalimisha kamanda wao Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na wasaidizi wake wakuu.

Akirekodiwa akiwa amevaa sare za kijeshi na kuzungukwa na wapiganaji wa RSF wenye furaha, Dagalo alisisitiza kwamba anataka amani irejee. Video ilichapisha Ijumaa.

Lakini hakukuwa na utulivu katika mapigano hayo ya Ijumaa, huku wananchi wakiripoti mashambulio ya anga na makombora katika maeneo yenye wakazi wengi wa mji mkuu Khartoum.

walioshuhudia pia waliripoti milipuko ndani ya kiwanda cha kutengeneza silaha cha Yarmouk.

Nchini kote, mapigano hayo yamesababisha vifo vya takriban watu 3,900 na kuwafukuza zaidi ya milioni 3.5 kutoka makwao.

TRT Afrika