Kampeni ya chanjo nchini kenya inalenga zaidi ya watoto milioni saba/ Picha: AP

Serikali ya Kenya inapanga kuanza kampeni dhidi ya polio nchini, awamu ya kwanza itakuwa kuanza tarehe 24 had 28 Agosti.

"Katika kampeni hii ya chanjo ya polio, tumeweka malengo yetu kuwafikia watoto milioni 7.4. " Mary Muthoni, katibu mkuu katika wizara ya afya ameambia washikadau mbalimbali amabao serikali imekutana nao kuwaelezea kuhusu kuunga mkono kampeni ya chanjo dhidi ya polio.

Chanzo zitapeanwa kupitia wahudumu kwenda nyumba kwa nyumba, katika taasisi za kidini na vituo vya afya. Itafanyika katika kaunti za Nairobi, Kiambu, Garissa na Kajiado.

"Awamu ya kwanza inalenga kaunti nne ya pili na ya tatu itafikia kaunti sita na lengo ni Kufikia zaidi ya 95% ya watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano," Daniel Langat, mkuu wa ufuatiliaji wa magonjwa katika wizara ya afya ya Kenya amesema.

Dkt, Patrick Amoth mkurugenzi mtendaji wa afya nchini Kenya anasema uhusiano kati ya milipuko wa polio na mabadiliko ya hali ya hewa unazidi kuwa wazi.

"Lengo letu lazima liwe katika utambulizi wa mapema wa visa vya polio . Huku nchi 33 zikiripoti kesi za polio, kampeni yetu ni thabiti katika kuwalinda watoto. Ili kuzuia milipuko hii, tunahitaji mifumo thabiti ya afya ya msingi ili kugundua visa hivi mapema," Dkt. Amoth amesema.

"Ni lazima tutetee watoto wetu wanufaike na sayansi inayopatikana. Chanjo ni salama. Wazazi, walezi na viongozi wa dini waungane kuhakikisha watoto wanapata chanjo."

TRT Afrika