Sheria mpya ya usalama barabarani itasaidia nchini Ghana?
AFRIKA
3 dk kusoma
Sheria mpya ya usalama barabarani itasaidia nchini Ghana?Bunge la Ghana limeidhinisha sheria mpya ya usalama barabarani inayojumuisha kuzingatia usalama wa watoto wanapokuwa kwenye gari.
Sheria mpya ya usalama barabarani nchini Ghana inajumuisha usalama wa lazima kwa watoto kulingana na umri, urefu, na uzito. / Wengine

Kwa Adwoa Mensah, maisha yake yalibadilika katika muda wa sekunde mbili.

“Tulikuwa tunaenda nyumbani Achimota. Binti yangu, Esi, ambaye ana umri wa miaka mitatu, ilikuwa nimemuweka kwenye mapaja yangu kiti cha nyuma sikutaka kumuamsha,” Adwoa mwenye umri wa miaka 31 ameielezea TRT Afrika, huku akicheza na mtoto wake.

“Alafu teksi iliokuwa mbele yetu ikasimama ghafla. Mume wangu akakanyaga breki. Esi akaruka kutoka kwenye mapaja yangu –na kichwa kikagonga kiti cha mbele kwa nguvu.”

Adwoa, mfanyabiashara katika soko la Makola jijini Accra. “Alilia kwa saa moja. Hakuvunjika mifupa, wala hakukuwa na damu. Lakini daktari alisema: ‘Kama ungekuwa umekanyaga breki baada ya mita kumi, au kama lori lingewagonga nyuma, binti yako angeruka kupitia kioo cha mbele. Kiti maalum cha mtoto kingesaidia kumfanya atulie kabisa.”

Hili lilifanyika mwishoni mwa mwaka 2025. Miezi miwili baadaye, bunge la Ghana limeidhinisha sheria mpya ya usalama barabarani, ambayo ilianza kutumika mwanzoni mwa 2026. Miongoni mwa masuala yanayotakiwa kuzingatiwa: usalama wa watoto kulingana na umri, urefu, uzito, na matatizo ya watoto wachanga na wadogo.

‘Helmet’ nyingi zinazouzwa hazijakidhi viwango vinavyohitajika, huku tafiti zikionesha kuwa waendesha pikipiki wengi wanatumia "helmet" ambazo viwango vyake ni vya chini, maarufu kama "bakuli", ambazo hazizingatii usalama.

Chini ya viwango hivyo vya sasa, ‘helmet’ zote za pikipiki zinazouzwa Ghana lazima ziwe kwa viwango vinavyohitajika.

‘Nunua kiti cha mtoto, mfunge mkanda’

Kwa msaada wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mradi wa Bloomberg Philanthropies kwa ajili ya Usalama Ulimwenguni, na washirika wengine, nchi zaidi ya 60 zimeimarisha sheria zake tangu 2007.

Hatua hii ya Ghana inakuja kabla ya Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuimarisha Usalama Barabarani Ulimwenguni, ambapo viongozi wa dunia watajadiliana kuhusu mipango yao ya kupunguza vifo na majeraha ya ajali barabarani kwa asilimia 50 kufikia 2030. Kote duniani, watu karibu miloni 1.2 hufariki kwa ajali kila mwaka, na ajali za barabarani zinaongoza kuwa chanzo cha vifo kwa watoto na vijana kati ya umri wa 5–29.

Tukirudi katika kizimba cha soko la Makola, Adwoa Mensah amemfunga binti yake Esi katika kiti kipya cha gari alichonunua – chenye rangi ya bluu.

“Mtizame,” Adwoa anasema, akitabasamu huku Esi akicheka na kutafuna mkanda. “Anadhani ni kiti cha malkia. Labda ndiyo hivyo. Pengine kiti hiki kidogo kinaweza kuwa sababu ya yeye kukua.”

Kabla hajaondoka kwa gari, Adwoa anahakikisha mkanda wa usalama wa Esi mara kadhaa, kuthibitisha kuwa amefungwa vizuri.

“Sheria ni nzuri. Lakini huwa namwambia kila mama mtoto ninayemuona: usisubiri mpaka polisi akusimamishe. Usisubiri upate ajali. Nunua hicho kiti. Mfunge mkanda mtoto. Hayo ndiyo mapenzi. Mengineyo ni kelele tu.”

CHANZO:TRT Afrika English