| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Uingereza yafikiria kurejea tena ndani ya Umoja wa Ulaya
Uingereza ilipiga kura ya kujiondoa ndani ya Umoja wa Ulaya, kupitia kura ya maoni ya mwaka 2016.
Uingereza yafikiria kurejea tena ndani ya Umoja wa Ulaya
Waziri Mkuu wa Uingereza, Andy Burnham.

Waziri Mkuu wa Uingereza Andy Burnham, amebainisha kuwa, uamuzi wa nchi hiyo kurejea ndani ya Umoja wa Ulaya, utasaidia katika kukuza mahusiano na mataifa mengine ndani ya umoja huo.

Akizungumza siku ya Jumatano, Burnham alisema kuwa anatumaini kuwa, Uingereza itarudi tena kwenye umoja huo.

"Kwa sasa, tunaangalia namna mbalimbali za kurudi ndani ya E, kwa kuzingatia faida na hasara zake,” alieleza.

Kulingana na Burnham, ambaye alishika wadhifa wa uwaziri mkuu kuanzia mwezi Julai mwaka huu, mchakato wa kujiondoa ndani ya Umoja wa Ulaya, maarufu kama ‘Brexit’, umeathiri nchi hiyo kwa kiasi kikubwa.

Uingereza ilipiga kura ya kujiondoa ndani ya Umoja wa Ulaya, kupitia kura ya maoni ya mwaka 2016.

CHANZO:AFP