| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia Oktoba 29
Tume hiyo inatarajiwa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio ya ghasia yaliyojitokeza wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Tanzania: Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia Oktoba 29
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania./Picha:@SuluhuSamia

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, ameunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya Ghasia yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Kwa mujibu wa taarifa wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi wa nchi hiyo Mei 18, 2026, hatua hiyo imechukuliwa katika kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Rais iliyochunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea kipindi cha uchaguzi huo, kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32.

Katika uteuzi huo, Jaji Shabani Ally Lila ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.
Wajumbe wengine walioteuliwa kuwa makamishna ni pamoja na Gad John Mjemmas, Awadh Mohamed Bawazir pamoja na Aishieli Nelson Sumari.

Tume hiyo inatarajiwa kufanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio ya ghasia yaliyojitokeza wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

CHANZO:TRT Afrika Swahili