tokea masaa 3
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe anaamini kuwa michuano ya AFCON 2027 itafanyika Afrika Mashariki, kama ilivyopangwa na wala haitohairishwa hadi mwaka 2028.
Akizungumza Februari 13, jijini Dar es Salaam, Motsepe alisisitiza kuwa kuwa ana imani na matayarisho yaliyofanywa na mashirikisho ya soka ya Tanzania, Kenya na Uganda kama wenyeji wa michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
“Nina imani kuwa michuano ya AFCON itafanyika hapa, kwahiyo sitaki kusikia swali la michuano ya AFCON kuhamishiwa sehemu nyingine,” alisema Motsepe.
“Tunafahamu kuna changamoto za hapa na pale, lakini ni muhimu kuendelea kuaminiana na kuungana mkono kama Waafrika, kwani inawezekana.”
CHANZO:TRT Afrika Swahili













