| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Rwanda ‘yahofia’ operesheni za DRC dhidi ya kikundi cha FDLR
Kulingana na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Olivier Nduhungirehe ahadi zitokanazo na mkataba wa amani wa Washington zitekelezwe kwa vitendo na si maneno tu.
Rwanda ‘yahofia’ operesheni za DRC dhidi ya kikundi cha FDLR
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe./Picha:@RwandaMFA
tokea masaa 2

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe ameonesha wasiwasi wake kufuatia operesheni zilizoendeshwa na jeshi la DRC za kuwapokonya silaha wapiganaji wa Jeshi la Kidemokrasia la Ukombozi wa Rwanda walioko DRC.

Uwepo wa wanajeshi wa FDLR nchini DRC, ni moja ya mambo yaliyoangaziwa katika mkataba wa amani wa Washington, uliosainiwa mwaka jana.

Akizungumza katika gwaride maalumu lililofanyika Kisangani siku ya Jumapili, Naibu Kamanda wa Majeshi ya DRC, Jenerali Jacques Ychaligonza aliwataka wapiganaji wa FDLR wasalimishe silaha zao kwa hiyari, ili kuepuka vifo zaidi katika eneo hilo.

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya maofisa wa DRC na Rwanda kukutana jijini Washington Machi 17 na 18 mwaka huu, kujadiliana namna ya utekelezwaji wa mkataba wa amani wa Washington.

Hata hivyo, kwa upande wake, Nduhungirehe alisema yupo tayari kuona utekelezaji wa vitendo na sio ahadi tu.

 

CHANZO:AA