Gaza residents fleeing

Jumamosi, Oktoba 13, 2023

Idadi ya Wapalestina waliouawa na mashambulizi makubwa ya anga ya Israel dhidi ya Gaza imeongezeka hadi 2,215, Wizara ya Afya ya Gaza ilisema.

Katika taarifa, wizara hiyo ilisema kuwa watoto 724 na wanawake 458 ni miongoni mwa watu waliouawa katika mashambulizi ya Israel.

Wizara pia imesema idadi ya waliojeruhiwa imefikia 8,714, wakiwemo watoto 2,450 na wanawake 1,536.

1022 GMT - Jeshi la Israel linasema wakazi wa Gaza hawapaswi 'kuchelewesha' kuhama

Msemaji wa jeshi Richard Hecht alisema kuna "dirisha" la kupita kwa usalama kuelekea kusini mwa Gaza kati ya 10:00 asubuhi na 4:00 jioni. Bila kusema ni siku ngapi dirisha lingesalia, Hecht aliwaambia waandishi wa habari: "Tunajua hii itachukua muda lakini tunapendekeza watu wasichelewe."

1018 GMT - Vifaa vya kibinadamu vilikatwa kutoka Ukanda wa Gaza kwa wiki moja: UN

"Limekuwa suala la kufa kupona. Ni lazima; mafuta yanahitajika kufikishwa sasa Gaza ili kufanya maji yapatikane kwa watu milioni 2," Philippe Lazzarini, kamishna mkuu wa UNRWA, alisema katika taarifa.

"Hakuna vifaa vya kibinadamu ambavyo vimeruhusiwa kuingia Gaza kwa wiki sasa," alisema.

0927 GMT - Ndege ilitua Misri ikiwa na vifaa vya matibabu vinavyohitajika sana kwa Gaza: WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa ndege iliyokuwa na vifaa vya matibabu vinavyohitajika sana kwa watu wa Gaza ilikuwa imetua Misri.

0848 GMT - Ndege ya Uturuki iliyobeba misaada ya kibinadamu kuelekea Gaza yawasili Misri

Ndege hiyo ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa El Arish nchini Misri, ambao ni jirani na eneo hilo la mapigano na imeutenga kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa Gaza.

0555 GMT - Jeshi la Israel lilidai kumuua kamanda mkuu wa kijeshi wa Hamas ambaye aliongoza operesheni za anga za kundi hilo huko Gaza.

Murad Abu Murad aliuawa siku iliyopita wakati ndege za kivita zilipopiga kituo cha operesheni cha Hamas ambapo kundi hilo liliendesha "shughuli zake za angani", jeshi lilisema Jumamosi.

Hakukuwa na uthibitisho kutoka kwa Hamas.

0401 GMT - Israel inaendelea kushambulia Gaza; Ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulizi makali kaskazini mwa Gaza mapema Jumamosi huku kukiwa na ripoti za majeruhi.

Mashambulio yao yalilenga nyumba na vifaa kadhaa katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia na kitongoji cha Al-Mashrooh huko Beit Lahia, kulingana na ripota wa Anadolu.

Makumi ya Wapalestina waliripotiwa kuuawa katika mashambulizi hayo. Wizara ya Afya ya Palestina bado haijathibitisha vifo hivyo.

Jeshi la Israel liliwaonya wakaazi milioni 1.1 kaskazini mwa Gaza kuhama siku ya Ijumaa "ndani ya saa 24" na kuelekea kusini kabla ya mashambulizi ya ardhini dhidi ya Hamas yanayotarajiwa.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa haitawezekana kwa Wapalestina huko Gaza kutii amri ya kuondoka kaskazini bila "matokeo mabaya ya kibinadamu."

TRT World