Wapalestina walivamia upande wa Israeli katika mpaka wa Israel na Gaza baada ya wapiganaji kujipenyeza katika maeneo ya kusini mwa Israel, Oktoba 7, 2023. / Picha: Reuters

Israel imetangaza 'hali ya kujitayarisha' kwa vita baada ya kundi tawala la Palestina Hamas kuanzisha operesheni ya kijeshi ambayo haijawahi kushuhudiwa dhidi ya Israel, na kujipenyeza kutoka baharini, nchi kavu na angani hadi katika maeneo ya makazi ya Israel chini ya maelfu ya maroketi.

Siku ya Jumamosi asubuhi, makumi ya wapiganaji wa Kipalestina walivamia kambi za Israeli katika eneo hilo, na kukamata vyombo vya usalama vya Israeli.

Redio ya Israel ilisema wapiganaji wa Hamas wamewateka Waisraeli 35.

Kiongozi wa mrengo wa kijeshi wa Hamas, Mohammed Deif, alitangaza kuanza kwa kile alichokiita "Operesheni Al Aqsa Dhoruba."

"Leo watu wanarejesha mapinduzi yao," alisema katika ujumbe huo uliorekodiwa, wakati akitoa wito kwa Wapalestina kutoka mashariki mwa Jerusalem hadi kaskazini mwa Israel kujiunga na vita na "kuwafukuza wavamizi na kubomoa kuta."

"Lazima tuwashe moto ardhi chini ya miguu ya wavamizi," alisema, akidai kuwa Hamas ilirusha zaidi ya makombora 5,000 ndani ya Israel.

Shambulio hilo linakuja baada ya Mpalestina mmoja kuuawa wakati wa mapigano na walowezi haramu wa Israel katika mji unaokaliwa wa Ukingo wa Magharibi wa Huwara, ambapo ghasia mpya zilizofanywa na walowezi wakati wa mazishi yake ziliwaacha wengine tisa hospitalini.

Milio ya roketi kutoka kwa eneo la Wapalestina lililozingirwa ilirushwa kutoka maeneo mengi kuanzia saa 06:30 asubuhi [0330 GMT] na kuendelea kwa karibu nusu saa, mwandishi wa habari wa AFP aliripoti.

Jeshi la Israel likuhuslitoa onyo kwa ving'ora kusini mwa nchi hiyo, huku polisi wakiwataka wananchi kukaa karibu na makazi ya mabomu. Milipuko ilisikika katika miji karibu na Tel Aviv na nje ya Yerusalemu inayokaliwa.

Israel imeweka vizuizi vinavyolemaza Gaza tangu mwaka 2007. Wapiganaji wa Palestina na wanajeshi wa Israel wamepigana vita kadhaa vikali tangu wakati huo.

Vikwazo hivyo vinavyozuia watu na bidhaa kuingia na kutoka Gaza, vimeharibu uchumi wa eneo hilo. Wapalestina wanasema kufungwa ni sawa na adhabu ya pamoja.

Israeli inatangaza ‘hali ya kuwa tayari’ kwa vita

Baada ya maroketi kutishia serikali ya Israel, ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ilitoa taarifa kwamba atawakutanisha maafisa wakuu wa usalama katika saa zijazo.

Jeshi la Israel liliripoti kuwa idadi kadhaa ya wapiganaji wa Kipalestina wamejipenyeza Israel kutoka baharini, nchi kavu na angani kutoka Gaza iliyozingirwa na kuwataka Waisraeli kuingia ndani ya nyumba zao.

Jeshi la Israel pia limesema liko katika mkondo wa vita na limeanza kulenga shabaha katika Gaza iliyozingirwa.

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant ameidhinisha kuitwa kwa wanajeshi wa akiba huku kukiwa na mapigano yanayoendelea.

Kuongezeka kwa idadi ya vifo

Takriban watu watano waliuawa na wengine 15 kujeruhiwa katika shambulio la roketi Gaza, Mamlaka ya Utangazaji ya Israel imeripoti.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 60 aliuawa "kutokana na mlipuko wa moja kwa moja" na wengine 15 walijeruhiwa kusini mwa Israel baada ya makumi ya roketi kurushwa kutoka kwenye eneo lililozingirwa, kulingana na taarifa ya huduma za dharura.

TRT World