Vifaru vya Israel vyaingia barabara kuu  ya mji wa Gaza: Mashahidi

Vifaru vya Israel vyaingia barabara kuu  ya mji wa Gaza: Mashahidi

Mashahidi wanasema vifaru vilionekana katika mtaa wa Salah Al-Din katika mji wa Gaza.
Kulingana na mashahidi, vifaru vya Israel vilionekana katika mtaa wa Salah Al-Din katika mji wa Gaza. Picha: AA

Mizinga ya Israel ilisukuma kuelekea ndani ya ukanda wa Gaza mashariki na kufikia barabara kuu katika jiji la Gaza, siku ya Jumatatu, mashahidi waliiambia Anadolu.

"Baadhi ya mizinga ya Israel na vifaru vilihamia Mashariki mwa Gaza na kufikia makutano ya Netzarim na barabara ya Salah Al-Din katika jiji la Gaza," walisema.

Vifaru hivyo vilihamishwa Jumapili usiku kutoka mji wa Juhor Ad-Dik ulioko mashariki mwa ukanda wa Gaza hadi barabara ya Salah Al-Din, kusini mashariki mwa Jiji la Gaza, kulingana na mashahidi.

Kwa mujibu wa mashuhuda, uvamizi huo pia uliambatana na makombora mazito na mashambulizi ya anga

Taarifa pia zinasema kwamba, gari la kivita la Israel liligonga gari lililokuwa likibeba familia ya Wapalestina waliokuwa wakihama kutoka kusini mwa Gaza kwenda mji mwengine.

Hakuna habari iliyopatikana kuhusu majeruhi.

Siku ya Ijumaa, jeshi la Israel lilipanua mashambulizi yake ya angani na ardhini katika Ukanda wa Gaza, ambao umekuwa chini ya mashambulizi ya angani tangu shambulio la ghafula la Hamas mnamo Oktoba 7.

Takriban watu 9,500 wameuawa katika mashambulizi hayo, wakiwemo Wapalestina 8,005, wengi wao wakiwa watoto na wanawake, na zaidi ya Waisraeli 1,538.

TRT World