Urusi imeishutumu Ukraine kwa kuishambulia Kremlin kwa kutumia ndege zisizo na rubani usiku kucha katika jaribio lililoshindwa la kumuua Rais Vladimir Putin.
Ikulu ya Kremlin ilisema siku ya Jumatano ndege mbili zisizo na rubani zilitumika katika shambulio linalodaiwa kuwa katika makazi ya Putin kwenye ngome ya Kremlin yenye ukuta, lakini zilizimwa na ulinzi wa kielektroniki.
Ilisema Urusi ilimejipanga kulipiza kisasi.
"Ndege mbili za angani ambazo hazikuwa na rubani zililenga Kremlin. Kutokana na hatua zilizo chukuliwa kwa wakati na jeshi la huduma maalum kwa kutumia mifumo ya vita vya rada, vifaa hivyo vilizimwa," ilisema taarifa ya Kremlin.
"Tunachukulia kitendo hiki kama kitendo cha kigaidi kilichopangwa dhidi ya uhai wa rais, kimefanywa usiku wa kuamkia Siku ya Ushindi, Parade ya Mei 9, ambayo uwepo wa wageni wa kigeni pia umepangwa ... Upande wa Urusi unahifadhi haki ya kuchukua hatua za kulipiza kisasi pale inapoona inafaa."
Ukraine ilisema "haina uhusiano wowote" na madai ya shambulio la ndege isiyo na rubani huko Kremlin.
"Ukraine haina uhusiano wowote na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani huko Kremlin," msemaji wa rais Mikhaylo Podolyak alisema. "Ukraine haishambulii Kremlin kwa sababu, kwanza, hiyo haisuluhishi malengo yoyote ya kijeshi," aliongeza.
Kufanya kazi kama kawaida'
Baza, chaneli ya Telegram yenye viungo vya mashirika ya kutekeleza sheria ya Urusi, ilichapisha video inayoonyesha kitu kikiruka kikikaribia jengo la Seneti ya Kremlin inayo tazamana na Red Square na kulipuka kwa mwanga mkali kabla ya kulifikia.
Taarifa kutoka kwa utawala wa rais ilisema vipande vya ndege hizo zisizo na rubani vimetawanywa kwenye eneo la jumba la Kremlin lakini hakukuwa na majeruhi au uharibifu wa mali.
Shirika la habari la RIA lilisema kuwa Putin hakuwa Kremlin wakati huo, na alikuwa akifanya kazi siku ya Jumatano katika makazi yake ya Novo Ogaryovo nje ya Moscow.
"Kutokana na kitendo hiki cha kigaidi, rais wa Shirikisho la Urusi hakujeruhiwa. Ratiba ya kazi yake haijabadilika, anafanya kazi kama kawaida," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema katika taarifa.
Kufuatia habari za jaribio la shambulio hilo, Moscow ilipiga marufuku safari za ndege zisizo na rubani katika mji mkuu.