Mwishoni mwa Mei, mawaziri wa ulinzi wa Urusi na Belarusi walitia saini makubaliano ya kupelekwa kwa silaha za nyuklia za Urusi huko Belarusi / Picha: Reuters

Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema Ijumaa kuwa uwekaji wa silaha za nyuklia nchini Belarus utaanza Julai.

Akizungumza katika mkutano na Rais wa Belarus Aleksandr Lukashenko huko Sochi, Putin alisema ujenzi wa vifaa maalum muhimu ili kupelekwa umepangwa kukamilika Julai 7-8.

“Kwenye masuala nyeti ambayo tumekubaliana kila kitu kinakwenda kwa mpangilio, mnavyofahamu maandalizi ya vituo husika yanaisha Julai 7-8, na mara moja tutaanza shughuli zinazo husiana na uwekaji wa aina husika ya silaha katika eneo lako," shirika la Anadolu limenukuu.

Mwishoni mwa Mei, mawaziri wa ulinzi wa Urusi na Belarusi walitia saini makubaliano ya kupelekwa kwa silaha za nyuklia za Urusi huko Belarusi, ambayo inaweka masharti ya kuziweka kwenye kituo maalum cha kuhifadhi.

Mapema mwaka huu, Putin alitangaza kwamba Urusi itapeleka zana za nyuklia na kukamilisha ujenzi wa kituo maalum cha kuhifadhi katika nchi jirani ya Belarus.

Putin alisema hatua hiyo ni katika kukabiliana na hatari zinazoongezeka za kiusalama, akisisitiza kwamba Moscow iliifuata Marekani, ambayo ilipeleka silaha zake za kiteknolojia za nyuklia katika nchi za Ulaya.

TRT Afrika