Wapalestina waanza kuhama baada ya Israel kushambulia Kambi ya Wakimbizi ya Nuseirat huko Gaza / Picha: AA

Jumapili, Julai 21, 2024

1111 GMT — Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea wasiwasi wake "mkubwa" juu ya uwezekano wa kuongezeka zaidi vurugu katika Mashariki ya Kati kufuatia uvamizi wa Israel kwenye bandari ya Al Hudaida magharibi mwa Yemen.

"Katibu Mkuu bado ana wasiwasi mkubwa juu ya hatari ya kuongezeka zaidi katika eneo hilo na anaendelea kuwahimiza wote kujizuia," ilisema taarifa iliyotolewa na ofisi ya mjumbe wake maalum kwa Yemen, Hans Grundberg.

Alitoa wito kwa pande zote zinazohusika "kuepusha mashambulizi ambayo yanaweza kuwadhuru raia na kuharibu miundombinu ya kiraia."

1233 GMT - Jeshi la Israeli latuma notisi y akuwasili kwa lazima waumini wa Orhtodox wa kiyahudi.

Jeshi la Israel limetoa notisi za kuwaita wanachama 1,000 wa jumuiya ya Orthodox katika hatua iliyokusudiwa kuimarisha safu ya jeshi lakini ambayo inaweza kuzidisha mvutano kati ya Waisraeli wa kidini na wasio na dini.

Mahakama ya Juu zaidi ilitoa uamuzi mwezi uliopita kwamba wizara ya ulinzi isingeweza tena kutoa msamaha wa jumla kwa wanafunzi wa seminari ya Kiyahudi kutoka kwa wanajeshi walioandikishwa.

Mpangilio huo ulikuwa umewekwa tangu wakati wa kuanzishwa kwa Israeli mnamo 1948 wakati idadi ya Waorthodoksi, au Haredi, ilikuwa ndogo.

Mabadiliko hayo mapya ya sera yamepingwa na vyama viwili vya kidini katika serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, na kuweka mvutano mkali katika muungano wa mrengo wa kulia huku vita vya Gaza vikiendelea.

1215 GMT - Wapiganaji wengine wawili wa Hezbollah waliuawa katika mapigano ya mpaka na Israeli

Wanachama wawili zaidi wa kundi la Lebanon la Hezbollah wameuawa katika mapigano na jeshi la Israel, kundi hilo limetangaza.

Katika taarifa tofauti, kundi hilo liliwataja wapiganaji waliouawa kuwa ni Mustafa Hassan Fawaz na Yassin Hussein Hussein.

Haikutoa maelezo kuhusu mazingira ya kifo chao, ikisema ni wao tu waliuawa "njiani kuelekea Jerusalem," kwa kurejelea mapambano ya Hezbollah ya kuunga mkono makundi ya upinzani ya Wapalestina yanayokabiliana na mashambulizi mabaya ya Israel huko Gaza.

Mauaji hayo mapya yalifikisha 375 idadi ya wapiganaji wa Hezbollah ambao wameuawa katika mapigano na wanajeshi wa Israel tangu Oktoba 8, 2023, kulingana na takwimu za Shirika la Anadolu.

1208 GMT - Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Israeli atoa wito wa 'kuharibiwa kabisa' kwa bandari ya Yemeni Hudaida

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman ametoa wito wa "kuharibiwa kabisa" kwa bandari ya Hudaida magharibi mwa Yemen.

"Lazima tuharibu kabisa bandari ya Al Hudaida," Lieberman, mkuu wa Chama cha Yisrael Beiteinu, aliiambia Redio ya Jeshi.

Alidai kuwa bandari hiyo ni "lango kuu la usambazaji wa silaha za Irani kwa Wahouthi."

1138 GMT - Iran inalaani shambulio la Israeli kwenye bandari ya Hudaida ya Yemen

Iran imelaani shambulio baya la Israel kwenye bandari ya Hudaida ambalo Wahouthi wanasema liliua watu sita na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Mwishoni mwa Jumamosi, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani "alilaani vikali" shambulio hilo akisema "ni kielelezo cha tabia ya kichokozi ya utawala wa Israel unaoua watoto."

Kanani aliongeza kuwa Israel na wafuasi wake, ikiwa ni pamoja na Marekani, "wanahusika moja kwa moja na matokeo hatari na yasiyotabirika ya kuendelea kwa uhalifu huko Gaza, pamoja na mashambulizi dhidi ya Yemen".

TRT World