Madhara ya mashumbuizi ya anga ya Israeli katika majengo eneo la Dahiyeh kusini mwa Beirut. /Picha: AA          

Chama cha Madaktari cha Lebanon kimeuomba Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuzuia "uharibifu" zaidi wa mfumo wa afya wa Lebanon unaofanywa na majeshi ya Israeli.

Siku ya Ijumaa, Shirika la Habari la Lebanon lilithibitisha kusimama kwa huduma katika hospitali za serikali za Marjayoun, Mays al Jabal na ile ya Salah Ghandoor kufuatia mashambulizi kutoka majeshi ya Israeli.

“Uhalifu unaoendelea dhidi ya sekta ya afya na timu za madaktari wa dharura vimefikia kiwango kikubwa, zikikiuka azimio la Haki la Binadamu la Umoja wa Mataifa, hususani kuhusu haki ya kupata huduma za afya,” kilisema chama hicho.

TRT Afrika