Idadi ya vifo kutokana na mfululizo wa matetemeko ya ardhi magharibi mwa Afghanistan ilivuka 1,000 Jumapili / Picha: AFP

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 lililofuatiwa na matetemeko mengine manane yenye nguvu na kutikisa maeneo mengi kufikia kilomita 30 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa mkoa wa Herat, likiangusha nyumba za vijijini na kuwafurusha wakazi wa jiji wenye hofu.

"Idadi ya vifo ni zaidi ya watu 1,000. Tunasubiri kuona jinsi takwimu za mwisho zitatokea. Kwa bahati mbaya, majeruhi ni wengi sana, kwani kiwango cha uharibifu kilikuwa wazi, " naibu msemaji wa serikali Bilal Karimi alisema mapema Jumapili akizungumza na AFP.

Shirika la afya duniani (WHO) lilisema kuwa zaidi ya nyumba 600 ziliharibiwa kabisa au kuharibiwa kwa sehemu katika vijiji 12 kwenye mkoa wa Herat, na jumla ya watu 4,200 kuathiriwa.

Hili Ni mojawapo ya matetemeko mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo katika miongo miwili.

WHO iliongeza Jumamosi "idadi ya majeruhi inatarajiwa kuongezeka zaidi huku shughuli za utafutaji na uokoaji zikiendelea".

Mkoa wa Herat yenye watu milioni 1.9 kwenye mpaka Na Iran, pia imekumbwa na ukame wa miaka mingi ambao umelemaza jamii nyingi zinazoshiriki kilimo huku hali ikiwa ngumu.

Zaidi ya watu 1,000 waliuawa na makumi ya maelfu kuachwa bila makao mwezi Juni mwaka jana baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.9 ambalo lilikuwa baya zaidi nchini Afghanistan takriban miaka 25, kupiga jimbo lenye umaskini la Paktika.

Baadhi wamenaswa katika vifusi

Awali mamlaka za mitaa zilitoa makadirio ya watu 100 waliouawa na 500 kujeruhiwa, kulingana na sasisho sawa kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu.

"Washirika na mamlaka za mitaa wanatarajia idadi ya waliopoteza maisha kuongezeka huku juhudi za utafutaji na uokoaji zikiendelea huku kukiwa na ripoti kwamba baadhi ya watu huenda wamenasa chini ya majengo yaliyoporomoka," Umoja wa Mataifa ulisema.

Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani limesema kuwa kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa takriban kilomita 40 kaskazini magharibi mwa mji wa Herat. Ilifuatiwa na mitetemeko mitatu yenye nguvu sana, yenye ukubwa wa 6.3, 5.9 na 5.5, pamoja na mishtuko midogo.

Shirika la Afya Duniani nchini Afghanistan limesema lilituma magari 12 ya ambulensi hadi Zenda Jan ili kuwahamisha majeruhi katika hospitali.

"Wakati vifo na majeruhi kutokana na tetemeko la ardhi wanaendelea kuripotiwa, timu ziko hospitalini kusaidia matibabu ya waliojeruhiwa na kutathmini mahitaji ya ziada," shirika la Umoja wa Mataifa lilisema kwenye X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter.

AFP