Papa Francis alichukua maamuzi ambayo hayajawahi kufanywa Jumatano hii kwa mkutano muhimu wa maaskofu, kwa kuwapa mara ya kwanza wanawake haki ya kupiga kura.
Papa aliidhinisha marekebisho ya kanuni zinazoongoza Sinodi ya Maaskofu, chombo cha Vatican kinachokusanya maaskofu wa dunia pamoja kwa mikutano ya mara kwa mara, Vatican ilisema katika taarifa yake.
Mabadiliko pia yanajumuisha kuruhusu ushiriki wa washiriki 70 wasio maaskofu - nusu yao wakiwa wanawake - katika sinodi iliyowekwa Oktoba.
Ikiwemo wanawake 10 kutapata kura.
Tangu Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikani, mikutano ya miaka ya 1960 iliyolifanya kanisa kuwa la kisasa, mapapa wamewaalika maaskofu kutoka kote ulimwenguni kwenda Roma kwa wiki chache kwa wakati mmoja ili kujadili maswala maalum.
Mwishoni mwa mikutano, maaskofu hupiga kura juu ya mapendekezo fulani na kuyaweka kwa papa, ambaye kisha huandaa hati inayozingatia mawazo yao.
Makundi ya wanawake wa kikatoliki kwa muda mrefu yamekosoa kanisa kwa kuwaweka wanawake nafasi ya pili. Walisifu mabadiliko ya papa kama hatua katika mwelekeo sahihi