Mabaki ya binadamu yaaminika kupatikana katika vifusi vya nyambizi ya Titan iliotoweka | Picha: reuters

Wataalam wameopoa mabaki yanayodhaniwa kuwa ya binadamu kutoka kwa kile kilichobaki cha chombo cha Titan kilichozama wakati wa uchunguzi wa eneo kulikotokea ajali ya Titanic, na kusababisha vifo vya watu watano, kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Pwani ya Marekani.

"Wataalam wa afya wa Marekani watafanya uchunguzi rasmi wa mabaki yanayodhaniwa kuwa ya binadamu ambayo yameopolewa kwa uangalifu," taasisi hiyo ilisema.

Katika chombo hicho walikuwemo mtafiti wa Uingereza Hamish Harding, mtaalamu wa vyombo vya chini ya maji kutoka Ufaransa Paul-Henri Nargeolet, tajiri wa Kipakistani-Muingereza Shahzada Dawood na mwanae Suleman, pamoja na Stockton Rush, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya OceanGate Expeditions inayosimamia chombo hicho.

AFP