Mwigizaji wa Kenya Lupita Nyong'o ameingia kwenye vitabu vya historia kwa kuwa mkuu wa kwanza mweusi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Berlin maarufu 'Berlinale'.
Tamasha la mwaka huu la "Berlinale" 2024, tamasha la kwanza la sherehe kubwa za filamu barani Ulaya mwaka huu, limeanza Februari 15 na litaendelea hadi Februari 25.
Aidha, ni makala ya mwisho chini ya uongozi wa sasa wa mkurugenzi mtendaji Mariette Rissenbeek na mkurugenzi wa sanaa Carlo Chatrian.
Lupita amesema alikuwa "ameheshimiwa sana" kutumikia kama rais wa waamuzi wa kimataifa na anatarajia "kusherehekea na kutambua kazi bora ya watengenezaji wa filamu kutoka kote ulimwenguni.”
Alinyakua Tuzo ya Oscar ya mwigizaji bora msaidizi mnamo 2014 kwa uigizaje wake katika filamu, "12 Years A Slave.”
Katika historia yake ya miaka 74, tamasha la Berlinale halijawahi kuwa na kiongozi mweusi wa jopo lake, na hivyo basi, Nyong'o atakuwa na wajibu muhimu wa kuchagua filamu bora katika vitengo vya Golden na Silver Bear.