Wapalestina watatu wameuwawa kufuatia shambulio la angani lilifanywa na vikosi vya Israeli katika mji wa Khan Younis, kusini mwa Gaza, shirika la habari la Wafa limeripoti.
Yassin Muhammad al-Amour, Mahmoud Adel al-Najjar, na mwanaye Adel waliuwawa katika shambulio hilo kwenye mji wa al Fukhari.
Watu wengine walijeruhiwa katika mashambulizi ya Israeli yaliyolenga nyumba mbili katika vitongoji vya vya Tuffah na al Shujaiya.
Vikosi vya Israel pia vilishambulia vitongoji vya Zeitoun, maeneo ya kaskazini mwa kambi ya Nuseirat, maeneo mengi ya Deir al Balah, mji wa Al-Masdar, na kambi ya Maghazi.
TRT Afrika