Watu 816, wakiwemo wanawake na watoto wameuwawa na wengine 2,507 wamejeruhiwa kupitia mashambulizi ya anga ya Israeli nchini Lebanon kuanzia Septemba 23, kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya ya Lebanon.
Jeshi la Israeli limeendelea kuongeza mashambulizi yake dhidi ya kile kinachokiita "Hezbollah", ikiwa ni ongezeko la mwaka mmoja wa vita vya kuvuka mpaka kati ya pande hizo mbili tangu Oktoba mwaka jana.
Kulingana na takwimu zilizoandaliwa na Shirika la Habari la Anadolu, watu 1,640 wameuwawa na wengine 8,408 wakijeruhiwa.
Idadi hiyo huenda ikaongezeka huku jeshi la Israeli likiendelea kufanya mashambulizi ya anga katika maeneo mbalimbali nchini Lebanon.
TRT Afrika