Jumamosi, Januari 25, 2025
09:12 GMT - Kundi la upinzani la Palestina Hamas limewakabidhi wanajeshi wanne wa Kiisraeli waliokuwa mateka huko Gaza kwa Msalaba Mwekundu.
0834 GMT - Hamas yatoa orodha ya wafungwa 200 wa Kipalestina watakaoachiliwa na Israel
Hamas ilitoa orodha ya wafungwa 200 wa Kipalestina wanaotarajiwa kuachiliwa na Israel badala ya wanajeshi wanne wa kike wa Israel kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya kundi hilo na Israel.
Wafungwa hao 200 ni pamoja na wafungwa waliotumikia kifungo cha muda mrefu na wengine wenye vifungo virefu.
0825 GMT - Hamas inawaomba Msalaba Mwekundu kujiandaa kwa uhamisho wa mateka: ripoti
Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ilipokea wito kutoka kwa Hamas kuelekea katika kituo maalum cha uhamisho huko Gaza ambako mateka wanne wa Israel wamepangwa kuachiliwa, Idhaa ya 12 ya Israel iliripoti.
Mwandishi wa Anadolu aliripoti kuwa majira ya asubuhi, msafara wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu uliondoka kuelekea kivuko cha Kerem Shalom kusini mwa Gaza.
Msafara huo ulikuwa na magari kadhaa ya Msalaba Mwekundu, likiwemo basi la kubeba watu 20-25. Bado hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu.
0818 GMT - Wanachama wa Hamas wanakusanyika katika medani ya Gaza kwa ajili ya kukabidhiana mateka
Wanachama kadhaa wa brigedi za Palestina za Al Qassam na Al Quds wamewasili katika uwanja muhimu kwenye mji wa Gaza, ambapo wanajeshi wanne wanawake wa Israel wanatarajiwa kukabidhiwa kwa Shirika la Msalaba Mwekundu, ripota wa AFP alisema.