Bangladesh kuongozwa na serikali ya muda baada ya Waziri Mkuu Hasina kujiuzulu

Bangladesh kuongozwa na serikali ya muda baada ya Waziri Mkuu Hasina kujiuzulu

Ripoti zinasema Sheikh Hasina amekimbilia jimbo jirani la Bengal Magharibi mwa India.
Ripoti zinasema Hasina ameondoka katika mji mkuu, Dhaka. / Picha: Reuters

Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina amejiuzulu, mkuu wa jeshi la nchi hiyo asema, akitangaza kuwa serikali ya mpito itasimamia masuala ya nchi hiyo hadi uchaguzi mpya ufanyike.

Mkuu wa Majeshi Waker-Uz-Zaman aliwataka waandamanaji hao kurudi nyumbani na kuwaruhusu wanajeshi kurejesha amani.

Maendeleo hayo yanamaanisha mwisho wa utawala wa miaka 15 wa Awami League, chama cha mwanzilishi wa jamhuri.

Ripoti zinasema Hasina, 76, alikimbilia jimbo jirani la Bengal Magharibi mwa India.

Ripoti za awali zilidokeza kwamba Hasina, pamoja na dada yake, waliondoka katika mji mkuu Dhaka huku kukiwa na maandamano makubwa.

"Yeye na dada yake wameondoka Ganabhaban (makazi rasmi ya Waziri Mkuu) kwenda mahali salama," chanzo kilisema. "Alitaka kurekodi hotuba. Lakini hakuweza kupata fursa ya kufanya hivyo."

TRT World