Uturuki  mara nyingi hutoa sauti ya kuunga mkono uadilifu na mamlaka ya eneo la Ukrainia, na haitambui unyakuzi haramu wa Crimea. / Picha: Reuters

Waziri wa nchi za kigeni wa Uturuki Hakan Fidan amekutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika ziara yake ya mji mkuu wa nchi hiyo, iliyoharibiwa na vita, Kiev.

Zelenskyy alisema kupitia taarifa yake kwenye mtandao wa Telegram ya kwamba, kufuatia mkutano wao wa siku ya Ijumaa, yeye na Waziri Fidan walijadili masuala mengi muhimu, ikiwa ni pamoja na mbinu ya amani aliyopendekeza katika mkutano wa hivi karibuni wa Kundi la G20 nchini Indonesia, maandalizi ya "Mkutano wa Amani wa Ulimwenguni" na "hatari zinazoletwa" kwa kizuizi cha Urusi cha ukanda wa nafaka wa Bahari Nyeusi."

"Ninaishukuru Uturuki kwa uungaji wake unaoendelea na thabiti kwa Ukraine!" Zelenskyy alisema.

Aidha, Katika ziara yake, Fidan alikutana pia na Waziri Mkuu Denys Shmyhal na kufanya mazungumzo na mkuu wa Ofisi ya Rais wa Ukraine Andriy Yermak. Vile vile, anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Ukraine Dmytro Kuleba.

Uturuki, inayosifiwa kimataifa kwa nafasi yake ya upatanishi kati ya Ukraine na Urusi, imetoa wito wa mara kwa mara kwa Kiev na Moscow kumaliza uhasama huo kupitia mazungumzo. Vita hivyo vimekuwa vikiendelea kwa zaidi ya siku 500.

Ankara ilitambua uhuru wa Ukraine mnamo1991, huku mahusiano kati ya Uturuki na Ukraine yakipata hadhi ya ushirikiano wa kimkakati mwaka wa 2011.

Kwa mara nyingi, Uturuki imetoa sauti ya kuunga mkono uadilifu na mamlaka ya eneo la Ukraine, na haitambui hatua isiyokuwa halali ya Urusi kunyakua Crimea mwaka wa 2014.

Uturuki mara nyingi hutoa sauti ya kuunga mkono uhuru wa eneo la Ukrainia, na haitambui hatua ya Urusi kunyakua Crimea mwaka wa 2014.

Mpango wa

nafaka

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amedokeza kuwa Fidan huenda akazuru Urusi hivi karibuni kwa minajili ya kufanya mazungumzo ya ana kwa ana.

Mwezi uliopita, Urusi ilisitisha ushiriki wake katika mpango wa nafaka wa Bahari Nyeusi, ambao ilitia saini msimu wa kiangazi uliopita pamoja na Uturuki , Umoja wa Mataifa, na Ukraine ili kuanza tena mauzo ya nafaka kutoka bandari tatu za Bahari Nyeusi za Ukraine.

Usafirishaji ulisitishwa mara tu baada ya vita vya Urusi na Ukraine kuanza mnamo Februari 2022.

Moscow imelalamika mara kwa mara kwamba upande wa Urusi wa makubaliano haukutimizwa

Ankara imekuwa ikifanya juhudi kubwa na kusukuma diplomasia kufanikisha kurejeshwa kwa mpango huo.

Siku ya Ijumaa, ikulu ya Kremlin ilisema kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin anatarajiwa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na Rais wa Uturuki Erdogan hivi karibuni.

Putin alimwambia Erdogan kupitia simu mnamo Agosti 2, kuwa Moscow iko tayari kurejea mkataba wa nafaka wa Bahari Nyeusi pindi tu nchi za Magharibi zitakapotimiza sehemu yao ya makubaliano kuhusiana na uuzaji wa nafaka yake.

TRT World