Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan siku ya Jumatano alihudhuria mkutano wa kikazi wa pamoja katika mji mkuu wa Niamey wa Niger.
Alisafiri katika taifa hilo la Afrika Magharibi katika ziara rasmi ya siku moja.
Fidan ameandamana na Waziri wa Ulinzi, Yasar Guler, Waziri wa Nishati na Maliasili Alparslan Bayraktar, mkuu wa ujasusi Ibrahim Kalin, Katibu wa Viwanda vya Ulinzi Haluk Gorgun na Naibu Waziri wa Biashara Ozgur Volkan.
Kikao hicho kiliongozwa na Waziri Mkuu wa Niger Ali Mahamane Lamine Zeine, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilisema kwenye X.
Duru za kidiplomasia siku ya Jumanne zilisema masuala yanaotarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo, ni uhusiano wa kisiasa na kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, matukio ya sasa hivi katika eneo la Sahel, na masuala ya kikanda, ikiwa ni pamoja na mzozo wa Israeli na Palestina.