Vikosi vya usalama vya Uturuki vimewakata makali magaidi wawili wa PKK kaskazini mwa Iraq, Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa imesema.
Magaidi hao walilengwa katika 'Operesheni Claw-Lock,' kulingana na Wizara hiyo siku ya Ijumaa.
"Tunaendelea kupambana na ugaidi kwa ufanisi na kwa uhakika katika chanzo chake," Wizara ilisema kwenye mtandao wa X.
Opereseheni ya Claw-Lock
Uturuki ilizindua Operesheni inayoitwa "Claw-Lock" mwezi Aprili 2022 ili kulenga maficho ya kundi la kigaidi la PKK katika maeneo ya Metina, Zap, na Avasin-Basyan kaskazini mwa Iraq, yaliyo karibu na mpaka wa Uturuki.
Mamlaka ya Uturuki hutumia neno "kukata makali" ikimaanisha magaidi wanaohusika walijisalimisha au waliuawa au kukamatwa.
Katika kampeni yake ya zaidi ya miaka 35 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na Umoja wa Ulaya - imehusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake, watoto na watoto wachanga.