Wizara ya afya ya Uturuki imesema kwa sasa hakuna haja ya vizuizi au hatua za ziada nchini. /Picha: AA

Kulingana na Wizara ya Afya ya Uturuki Hakuna maambukizi ya Mpox nchini Uturuki, ugonjwa huo ambao unaoedelea kusamabaa hasa katika bara la Afrika.

Kupitia ukurasa rasmi wa mtandao wa kijamii wa X, wizara hiyo imesema kwa sasa hakuna haja ya vizuizi au hatua za ziada nchini.

Wizara ya Afya inatekeleza kazi muhimu, na mchakato huo unafuatiliwa kwa karibu, iliongeza katika taarifa hiyo.

Tangazo hilo lilikuja baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) siku ya Jumatano kutangaza hali ya mpox kuwa "dharura ya afya kwa umma na wasiwasi wa kimataifa."

Tangu mwanzoni mwa 2024, zaidi ya nchi kumi na mbili za Kiafrika zimeripoti ugonjwa huo, ambao huenezwa kwa mgusano, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikichukua zaidi ya 90% ya maambukizi hayo yaliyoripotiwa.

Kulingana na WHO, mpox husababisha upele na dalili zake ni kama dalili za mafua.

TRT World