Wizara ya Ulinzi ya Taifa la Uturuki imesema kuwa vikosi vya Uturuki viliharibu maeneo 32 ya magaidi katika operesheni ya anga iliyotekelezwa kaskazini mwa Iraq na Syria, na idadi kubwa ya magaidi "walikatwa makali."
Wizara hiyo ilisema katika taarifa yake siku ya Jumatano kwamba operesheni hiyo iliendeshwa kwa mujibu wa haki halali ya kujilinda, iliyotokana na Kifungu cha 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kwa lengo la "kukata makali" PKK/KCK na makundi mengine ya kigaidi ili kumaliza mashambulizi ya kigaidi dhidi ya umma na vikosi vya usalama na kuhakikisha usalama wa mpaka.
Taarifa hiyo ilisema malengo 32 ya magaidi yaliharibiwa kwa mafanikio na kwamba operesheni za anga zinaendelea madhubuti.
"Vikosi vya Wanajeshi wa Uturuki, vinavyotokana na taifa letu tukufu, vitaendeleza mapambano dhidi ya ugaidi kwa udhabiti na dhamira kwa ajili ya ustawi na usalama wa nchi na taifa letu hadi pale hakutakuwae na gaidi hata mmoja, kama ilivyokua hapo zamani.
"Wakati wa operesheni hizi, hatua zote muhimu zimechukuliwa ili kuhakikisha kuwa raia wasio na hatia, watu marafiki, maeneo ya kihistoria na kitamaduni na mazingira hazipati madhara," iliongeza.
Haya yanajiri baada ya shambulio la kigaidi katika vituo vya tasnia ya anga ya Uturuki siku ya Jumatano katika mji mkuu, Ankara.
Magaidi wawili waliohusika katika shambulio kwenye vituo hivyo "walikatwa makali," huku raia watano wakiuawa kishahidi na wengine 22 kujeruhiwa, Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Yerlikaya aliripoti.