Rais wa uturuki Recep Tayyip Erdogan ameeleza kuwa Uturuki itachukua hatua pamoja na Misri kupingwa kuhamishwa kwa nguvu kwa Wapalestina kutoka ardhi zao.
"Israel inawalazimisha watu wa Gaza kuishi kwa njaa. Lengo letu ni kufikia kusitisha mapigano mara moja na kuhakikisha misaada ya kibinadamu isiyokatizwa kwa Gaza, " Erdogan alisema Ijumaa, akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Kaskazini wa Giresun nchini Uturuki.
Akiangazia ziara za hivi karibuni UAE na Misri "zilizofanikiwa sana," rais Recep Tayyip Erdogan amesisitiza haja ya "kuungana" ili kukomesha umwagaji damu Gaza.
"Mbali na biashara na uwekezaji, tulijadili kwa undani suala la Palestina na wakuu wa nchi. Tumeamua kuimarisha ushirikiano wetu na nchi zote mbili, " alisema.
Akielezea kuwa Uturuki imekuwa ikituma misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza tangu Oktoba 7, Erdogan alisema kuwa Ankara daima imeshirikiana na mamlaka ya Misri kwa utoaji wa misaada ya kibinadamu Gaza.
"Kama ulimwengu wa Kituruki na Kiislamu, tutaendelea na mapambano yetu ya haki katika umoja, mshikamano na ushirikiano," Erdogan alisema, akitaka juhudi za misaada kwa gaza, haswa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Akisisitiza kwamba wanataka "Karne ya Uturuki" pia kuwa karne ya amani, rais wa Uturuki alielezea kuwa Ankara itafanya kazi ili kuboresha ushirikiano na nchi za kirafiki na za kindugu.
"Tunalazimika kuungana na nchi za ndugu ikiwa tunataka kuzuia michezo ya nguvu za kibeberu katika maeneo yetu.
Badala ya kukwama katika tofauti za mawazo, lazima tuzingatie maeneo ya ushirikiano. Sote tunajua ukweli huu: hakuna huruma bila umoja, " rais wa Uturuki alisema.