Baada ya kufuatilia kwa karibu kesi hiyo na kufanya tathmini za kina kuhusu uwezekano wa kujiunga na kesi dhidi ya Israeli, Uturuki alitangaza uamuzi wake wa kujiunga na kesi hioMei 1./ Picha: AFP

Uturuki imewasilisha ombi lake kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kujiunga na kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israeli, ikitaka kuiwajibisha Tel Aviv kutokana na uhalifu wake wa kivita vinavyoendelea dhidi ya watu wa Palestina huko Gaza inayozingirwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan alitangaza kuhusu rufaa hiyo siku ya Jumatano.

"Ikitiwa moyo na hali ya kutoadhibiwa kufuatia uhalifu wake, Israeli inazidi kuwaua Wapalestina wasio na hatia kila siku," Fidan aliandika kwenye X, akilaani ukatili usiokoma wa Israeli.

"Jumuiya ya kimataifa lazima iwajibike kukomesha mauaji ya kimbari na kuweka shinikizo linalohitajika kwa Israeli na wafuasi wake," aliongeza, akiahidi kwamba Uturuki "itafanya kila juhudi" kwa ajili hiyo.

Afrika Kusini imewasilisha kesi ICJ mwishoni mwa mwaka jana, ikisema kwamba vita vya uharibifu vya Israeli vimesababisha mgogoro wa kibinadamu na kukiuka Mkataba wa Mauaji ya Kimbari ya 1948. Nchi kadhaa zimejiunga na kesi hiyo.

Baada ya kufuatilia kwa karibu kesi hiyo na kufanya tathmini za kina kuhusu uwezekano wa kujiunga, Uturuki alitangaza uamuzi wake wa kuingilia kati Mei 1.

Nchi hiyo sasa imejiunga na kesi ya mauaji ya kimbari, ikiungana na Nicaragua, Colombia, Libya, Mexico, Palestina, na Uhispania, ambazo pia zimejiunga na Afrika Kusini, ambayo iliwasilisha kesi hiyo kwa mara ya kwanza Desemba mwaka jana.

Kujitolea kutetea haki

"Uamuzi wetu wa kujiunga na kesii unaonyesha umuhimu ambao nchi yetu inazingatia kupatikana suluhu kuhusu suala la Palestina kutumia mfumo wa sheria na haki," Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilisema katika taarifa kufuatia ombi hilo.

"Dhamira ya ubinadamu na sheria za kimataifa zitawajibisha maafisa wa Israeli," ilisisitiza.

Inaweza kuchukua miaka minne hadi mitano kabla ya ICJ kutoa uamuzi wa mwisho, lakini hoja ambazo pande tofauti kwenye kesi huwasilisha zinaweza kuwa msingi wa kuzuia uhalifu kama huo katika siku zijazo.

Mwezi uliopita, ICJ ilitoa ushauri wa kihistoria, ikiiambia Israeli kwamba kukalia kwa mabavu maeneo ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi, Jerusalem Mashariki na Gaza na ujenzi wa makaazi ni kinyume cha sheria.

Uturuki inasema kwamba hoja zake za kisheria zitaunga mkono maoni ya ICJ juu ya ukaliaji wa maeneo ya Palestina na makazi haramu.

Kulingana na maafisa wa kidiplomasia wa Uturuki, "Tamko la Uturuki ni la kina na pana zaidi, na linalojadiliwa vyema kati ya nchi zilizojiunga na kesi."

TRT World