Uturuki inaongoza duniani kwa kutuma misaada Gaza, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema.
Hadi sasa, tani 50,000 za misaada ya kibinadamu zimetumwa katika eneo lililozingirwa ambako mashambulizi ya Israeli yanaendelea, alisema Erdogan siku ya Jumatatu katika mkutano mjini Ankara.
"Uturuki inaongoza katika kutuma msaada mkubwa zaidi Gaza, ambapo jumla ya tani 50,000 za misaada ya kibinadamu zimetumwa hadi sasa," alisema.
Erdogan pia aliongeza kuwa, pamoja na serikali yake, raia, na mashirika yasiyo ya kiserikali, imejitokeza kama taifa inayokabiliana na kusaidia zaidi na changamoto zinizokabili Gaza.
Vita vya kikatili vya Israel dhidi ya Gaza
Israeli imeshambulia Gaza kwa kulipiza kisasi shambulio la Hamas tarehe 7 Oktoba mwaka jana, ambalo liliua takriban watu 1,200. Wapalestina takribani 34,700 wameuawa na wanajeshi wa Israeli huko Gaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na wengine 78,000 kujeruhiwa, kwa mujibu wa mamlaka ya afya ya Palestina.
Takriban miezi saba baada ya vita vya Israel, maeneo makubwa ya Gaza yalikuwa magofu, na asilimia 85 ya wakazi wa eneo hilo kuwa wakimbizi wa ndani huku kukiwa na uhaba wa chakula, maji safi na dawa, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Israeli inashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki. Uamuzi uliyotoka Januari ulisema "inawezekana" kwamba Israeli inafanya mauaji ya halaiki huko Gaza na kuiamuru Tel Aviv kukomesha vitendo kama hivyo na kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa msaada wa kibinadamu unatolewa kwa raia huko.