Uturuki inalenga kuongeza biashara yake na bara la Afrika hadi dola bilioni 50 za Marekani, karibu mara 10 ya takwimu ya mwaka 2003 ya dola bilioni 5.4, makamu wa rais wa nchi hiyo amesema.
Kiwango cha biashara kati ya Uturuki na nchi 54 za Afrika kimeongezeka mara saba, na kufikia dola bilioni 37 kutoka 2003 hadi 2023, Cevdet Yilmaz alisema baada ya mkutano na Waziri Mkuu wa Lesotho Samuel Ntsokoane Matekane katika mji mkuu wa Uturuki Ankara siku ya Jumanne.
Akiangazia uwekezaji wa Uturuki barani Afrika, Yilmaz alisema wawekezaji kutoka nchi yake wamechangia takriban dola bilioni 10 kwa bara hilo. Pia alisisitiza mafanikio ya makampuni ya kandarasi ya Uturuki, ambayo yametekeleza miradi 1,977 yenye thamani ya dola bilioni 91.6 barani Afrika. "Kiwango chetu cha biashara na nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kilipanda kutoka dola bilioni 1.35 mwaka 2003 hadi dola bilioni 12.4 mwaka 2023. Wakandarasi wa Uturuki wamefanya miradi 445 yenye thamani ya jumla ya dola bilioni 26.7 katika eneo hili," alisema. Akikubali kuwepo kwa maendelo kwa kiasi kidogo katika mahusiano ya biashara na uwekezaji na taifa la Kusini mwa Afrika Lesotho hapo awali, Yilmaz alionyesha matumaini ya enzi mpya kufuatia ziara ya Matekane.
“Ziara hii ya Waziri Mkuu Matekane ni ya kihistoria, inaashiria ziara ya ngazi ya juu kutoka Ufalme wa Lesotho katika nchi yetu. Ninaamini itakuwa muhimu katika kuendeleza mahusiano yetu na kuimarisha ushirikiano wa hali ya juu katika siku zijazo,” Yilmaz alisema.
Yilmaz alisisitiza dhamira ya Uturuki ya kusaidia maendeleo ya Afrika katika nyanja zote, akisisitiza ushirikiano unaojengwa juu ya udugu.
Aliangazia mtandao mpana wa Shirika la Ndege la Uturuki, na safari za ndege kwenda kwenye vituo zaidi ya 60 katika bara zima, na uwepo hai wa taasisi na wakfu wa Uturuki.
"Ili kuimarisha uhusiano wetu na Afrika, tumeongeza idadi ya balozi zetu kutoka 12 mwaka 2002 hadi 44 leo," alisema. Akibainisha kuwa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametembelea nchi 31 za Afrika hadi sasa, Yilmaz alisema juhudi za Ankara za "kupanua mtandao wetu wa kidiplomasia barani Afrika" ni pamoja na mji mkuu wa Lesotho Maseru. "Tunafuraha kufahamishwa kuhusu nia ya mamlaka ya Lesotho ya kufungua ubalozi huko Ankara siku zijazo," aliongeza.
Misheni za Kidiplomasia
Waziri Mkuu Matekane alisema kuwa ujumbe wake umeangalia kwa karibu maendeleo ya Uturuki katika sekta ya viwanda na teknolojia, akibainisha: "Tunaamini kwamba mwenendo huu utachukua nafasi muhimu sana katika mabadiliko ya kiuchumi ya nchi yetu."
Matekane alisisitiza umuhimu wa kihistoria wa ziara yake na kusema mataifa hayo mawili yalifanya mijadala muhimu yenye lengo la kuimarisha uhusiano wao.
Alisisitiza maeneo ya kimkakati ya ushirikiano, ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, kilimo, nishati, elimu, kujenga uwezo, utalii, na utamaduni, pamoja na ushirikiano katika uhamiaji na kazi.