Polisi mjini Istanbul wamewakamata watu 17 kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Daesh, duru za usalama zilisema siku ya Ijumaa.
Washukiwa hao, ambao wanaaminika kufanya kazi kama sehemu ya kundi la kigaidi na kusafiri kwenda na kutoka maeneo yenye migogoro, walikamatwa katika operesheni iliyoanzishwa katika wilaya nne za mji mkuu wa Uturuki.
Haya yalisemwa na vyanzo ambavyo viliomba kutotajwa jina kutokana na vikwazo vya kuzungumza na vyombo vya habari,
Mnamo 2013, Uturuki ilikuwa moja ya nchi za kwanza kutangaza Daesh kuwa shirika la kigaidi.
Tangu wakati huo nchi hiyo imeshambuliwa na kundi hili la kigaidi mara kadhaa, huku zaidi ya watu 300 wakiuawa na mamia zaidi kujeruhiwa katika milipuko 10 ya kujitoa mhanga, mashambulizi saba ya mabomu na mashambulizi manne ya silaha.
Na hapo Uturuki ilianzisha operesheni ya kupambana na ugaidi ndani na nje ya nchi ili kuzuia mashambulizi zaidi.