Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun anasema Ankara inatumai kwa dhati kwamba sheria mpya ya kupambana na ugaidi, ambayo itaanza kutumika Juni 1, itatekelezwa ipasavyo. / Picha: AA

Uhuru ambao kundi la kigaidi la PKK/YPG linao wa kuendesha shughuli zake nchini Sweden "haukubaliki kabisa," mkurugenzi wa mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun amesema.

"Haikubaliki kabisa kwamba magaidi wa PKK wanaendelea kufanya kazi kwa uhuru nchini Sweden- ambayo imetuma ombi la uanachama wa NATO," Altun alisema katika tweet Jumanne.

"Jana usiku, walionyesha kile kinachoitwa bendera ya PKK kwenye bunge la Sweden, " Altun alisema Ankara inatarajia mamlaka ya Sweden "kuchunguza tukio hilo, kuwawajibisha wale waliohusika na kuacha wanachama wanaojitambulisha wa PKK kufanya kazi nchini Sweden, PKK inatambuliwa na umoja wa ulaya kama taasisi ya kigaidi,"

Matamshi yake yanajiri baada ya video katika mitandao ya kijamii zilionyesha kijitambaa kinachoashiria kundi hilo la kigaidi la PKK/YPG jijini Stockholm kuonekana mbele ya bunge la taifa la Sweden.

Wafuasi wa PKK/YPG pia walisambaza video zenye uchochezi dhidi ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson na Waziri wa Mambo ya Nje Tobias Billstrom.

Katika mojawapo ya video hizo, wafuasi wa PKK/YPG waliwatusi maafisa hao wawili wa Sweden na kuchoma moto bango la Erdogan.

Maandamano yajayo

Magaidi hao walitangaza maandamano jijini Stockholm kupinga sheria mpya ya kupambana na ugaidi ambayo itaanza kutumika tarehe 1 Juni.

Sheria hiyo inalenga kufanya haramu uanachama katika mashirika ya kigaidi nchini na inaipa mamlaka nchini uwezo mkubwa zaidi ya kuwakamata na kuwashtaki watu wanaofadhili au kuunga mkono mashirika ya kigaidi.

"Tunatumai kwa dhati kwamba sheria mpya ya kupambana na ugaidi, ambayo itaanza Juni 1, itatekelezwa ipasavyo. Mamlaka nchini Sweden lazima izuie wanachama wa PKK kuandamana Juni 4 ikiwa wana nia ya dhati kushughulikia wasiwasi wa Uturuki," Altun alisema.

Katika kampeni yake ya ugaidi ya takriban miaka 40 dhidi ya Uturuki PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, Uingereza na umoja wa ulaya.

Kundi hilo limehusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake, watoto na watoto wachanga. Wana tawi kaskazini mwa Syria linayojulikana kama YPG.

TRT World