Ujumbe huo unatarajiwa kudumu takriban miezi saba na utahusisha kukusanya data ya mitetemo ya mafuta na gesi asilia. / Picha: Kumbukumbu ya AP

Meli ya utafiti ya Uturuki, Oruc Reis, imewasili katika pwani ya Somalia kwa ajili ya tafiti za jiolojia kuhusu uwepo mafuta, na gesi asilia, Waziri wa Nishati na Maliasili wa Uturuki Alparslan Bayraktar alitangaza.

"Oruc Reis imefikia eneo lake la misheni baada ya safari yake iliyopitia mabara kadhaa," Bayraktar alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X siku ya Ijumaa.

Waziri huyo pamoja na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud watahudhuria hafla ya kukaribisha meli ya tafiti za jiolojia baadaye mchana.

Meli hiyo ilianza safari kuelekea Somalia mapema mwezi huu kwa ajili ya shughuli za uchunguzi wa mafuta, gesi asilia na mitetemo katika maeneo matatu matatu ambayo Uturuki imepata leseni za utafutaji.

Oruc Reis itafanya tafiti za jiolojia kuhusu uwepo wa gesi asilia katika maeneo matatu ya pwani ya Somalia.

Misheni hiyo inatarajiwa kudumu takriban miezi saba na utahusisha kukusanya data ya mitetemo, mafuta na gesi asilia.

Data hii itachambuliwa mjini Ankara ili kutambua maeneo yanayoweza kuchimba visima.

Hati za makubaliano

Mapema mwaka huu, Uturuki na Somalia zilitia saini hati za makubaliano kati ya wizara zao na serikali.

Chini ya makubaliano haya, 'Turkish Petroleum', kampuni ya kitaifa ya mafuta ya Uturuki, ilipata leseni kwa maeneo matatu ya pwani ya Somalia.

Wizara inapanga kufanya tafiti za jiolojia katika kanda tatu zenye leseni, kila moja ikichukua takriban kilomita za mraba 5,000 (maili za mraba 1,931).

TRT World