Maandamano ya kuunga mkono Palestina yatafanyika katika zaidi ya majimbo 60 huko Uturuki

Maandamano ya kuunga mkono Palestina yatafanyika katika zaidi ya majimbo 60 huko Uturuki

Mashirika ya kiraia kuandamana barabarani kuonyesha mshikamano na Wapalestina huku kukiwa na hali mbaya zaidi ya mgogoro huko Gaza.
Maandamano huko Ankara yataanza saa saba za mchana, kutoka Hifadhi ya Kurtulus hadi Anadolu Square, na karibu washiriki milioni 1 wanatarajiwa. / Picha: Jalada la AA

Maandamano ya kuunga mkono Palestina yatafanyika katika zaidi ya majimbo 60 kote Uturuki Jumapili hii, huku kukiwa na hali mbaya ya mzozo huko Gaza.

Yakiwa yameandaliwa na Jukwaa la Mashirika ya Kiraia ya Anatolia, matukio haya yanalenga kuangazia hali mbaya zaidi ya kibinaadamu huko Palestina kutokana na mashambulizi yanayotekelezwa na Israeli tangu Oktoba mwaka jana.

Metin Mahitapoglu, mjumbe wa bodi ya jukwaa hilo, alisema kuwa Israeli imezidisha mashambulizi yake kwa kuungwa mkono na Marekani, Uingereza, na Umoja wa Ulaya, na kuendeleza mashambulizi zaidi ya Gaza hadi nchi nyingine, kama Lebanon, Syria, Yemen na Iran, katika eneo hilo.

Alibainisha kuwa mashirika ya kiraia yataingia mitaani kuonyesha mshikamano na Palestina na kuwafichua "wale walioshiriki katika ghasia."

Mahitapoglu pia alitangaza kuwa maandalizi yanaendelea kwa ajili ya maandamano katika majimbo yote 81, huku maandamano makubwa yakipangwa katika mji mkuu Ankara.

"Lazima tujiandae kwa kile ambacho kinaweza kufikia mlango wetu hivi karibuni"

"Licha ya mauaji ya kimbari na uharibifu unaoendelea, lazima tujiandae kwa kile ambacho kinaweza kufikia mlango wetu hivi karibuni. Lazima tuungane na moyo wa upinzani wa kitaifa dhidi ya mawazo ya kibeberu ambayo yanadai kuwa taifa linalokalia kwa mabavu la Israel lina haki ya kujilinda.

Tunatoa wito kwa dunia na watu wote wenye dhamiri: Jiunge na maandamano, ingia mitaani, na kususia bidhaa za makampuni yanayounga mkono Israeli ya Kizayuni,” alisema.

Maandamano huko Ankara yataanza saa saba za mchanam saa za Uturuku, kutoka Hifadhi ya Kurtulus hadi Anadolu Square, na karibu washiriki milioni 1 wanatarajiwa.

Maandamano hayo yanaungwa mkono na makundi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, vyama vya wafanyakazi, na jumuiya za kidini, na zaidi ya hatua 400 za mshikamano tayari zimeandaliwa na mashirika ya kiraia ya Ankara, kulingana na Mahitapoglu.

TRT World