Rais Erdogan anabainisha OTS imekuwa na jukumu kubwa katika kuimarisha uhusiano kati ya mataifa ya Turkic na kuongeza ushirikiano, na kuchangia katika kukua kwa ushikamano kati ya watu wa Kituruki. / Picha: AA

Kitabu kipya cha Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki kimeangazia uhusiano wa Uturuki na nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Turkic (OTS), ilisema.

'The Shining Star of the 21st Century: Organization of Turkic States' yaani 'Nyota Ing'aayo ya Karne ya 21: Shirika la Nchi za Turkic lilitayarishwa kwa mkutano wa 10 wa OTS katika mji mkuu wa Kazakhstan wa Astana.

Kitabu hicho kinaonyesha uhusiano thabiti wa urafiki na udugu katika uchumi, utamaduni, usafiri, nishati, afya, elimu, vyombo vya habari, sayansi na teknolojia ambavyo vimebuniwa tangu zamani hadi sasa, ilisema Ijumaa.

Kinajumuisha mshikamano wa kibinadamu ulioonyeshwa na nchi za Turkic na wananchi wao wakati wa janga la Uviko 19, vita vya pili vya Karabakh na mitetemeko mbili ya ardhi kusini mwa Uturuki mnamo Februari 6.

Kitabu hiki kina sehemu tatu: Shirika la nchi za Turkic kama Taasisi, umoja wa siku za zamani , siku zijazo zenye nguvu - Maeneo ya Ushirikiano katika nyakati ngumu.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisisitiza umuhimu ya kuimarisha uhusiano na undugu kati ya watu wa mataifa ya Turkic ambayo yana mizizi moja, historia na utamaduni, kusimama pamoja wakati wa furaha na huzuni.

Erdogan alibainisha OTS imekuwa na jukumu kubwa katika kuimarisha uhusiano kati ya mataifa ya Turkic na kuongeza ushirikiano, na kuchangia katika kukua kwa mshikamano kati ya watu wa Turkic.

Nchi wanachama wa OTS zimekuwa zikipambana na ugaidi, chuki dhidi ya watu wa Turkic na dhidi ya Uislamu, aliongeza.

TRT Afrika