Uturuki inafuatilia kwa karibu yanayoendelea Syria na kuwa inachukua hatua madhubuti kusitisha mapigano kati ya utawala wa Bashar al Assad na vikundi vyenye silaha nchini humo, amesema Rais Recep Tayyip Erdogan amesema.
"Tunafuatilia kwa karibu yanayojiri huko Syria" alisema Erdogan katika mkutano wa wanahabari akiwa na kiongozi mwenzake Jakov Milatovic wa Montenegro, katika mji mkuu wa Ankara nchini Uturuki siku ya Jumatatu.
Kulingana na Erdogan, Ankara inafuatilia kwa karibu kile kinachoendelea Syria kama ilivyo kipaumbele chake cha usalama na kuwa inachukua hatua madhubuti kuepusha madhara zaidi.
"Ni hamu yetu kuona kuwa utawala wa Syria unahifadhiwa na kulingana na mahitaji ya watu wa Syria," alisema Rais Recep Tayyip Erdogan.
Alisisitiza kuwa Ankara iko tayari kumaliza kila aina ya mapigano katika kanda yake.
Mapigano yalizuka tarehe 27 Novemba kati ya wanajeshi wa utawala wa Assad na makundi yanayopinga serikali katika eneo la mashambani la Aleppo kaskazini mwa Syria, na kuashiria kuongezeka tena kwa mapigano hayo baada ya kipindi cha utulivu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoikumba Syria tangu mwaka 2011.