Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema kuwa anaamini kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin anataka kuendelea kwa makubaliano ya kuruhusu usafirishaji wa nafaka za Ukraine kupitia Bahari Nyeusi baada ya Moscow kusema kuwa itasitisha ushiriki wake.
Akizungumza na waandishi wa habari, Erdogan alisema atazungumzia mpango huo, ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa mbolea ya Urusi, na Putin watakapokutana ana kwa ana wakati wa mkutano unaotarajiwa mwezi Agosti.
Lakini aliashiria kwamba anaweza kujadiliana na rais wa Urusi kwa njia ya simu bila kungoja mkutano wa Agosti.
Uturuki daima imetilia maanani uendelezaji wa mpango wa nafaka wa Bahari Nyeusi na imeongeza juhudi za kidiplomasia, Rais Erdogan alisema.
TRT Afrika