Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekutana na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau kando ya mkutano wa NATO unaoendelea huko Vilnius, mji mkuu wa Lithuania.
Mkutano huo wa faragha ulifanyika katika Kituo cha Maonyesho cha Lithuania na Congress, ukumbi wa mkutano wa siku mbili wa NATO ulioanza Jumanne.
Hapo awali, Erdogan pia alikutana na kiongozi mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak.
Viongozi 31 wa muungano wa kijeshi wanakutana kujadili mzozo wa Urusi na Ukraine, pendekezo la NATO la Sweden, na hatua za kuimarisha ulinzi na usalama nakuzuia mashambulio, miongoni mwa masuala mengine.
Recep Tayyip Erdogan pia anatarajiwa kukutana na viongozi wengine wa nchi za NATO, akiwemo Rais wa Marekani Joe Biden na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis.
Uturuki imekuwa mwanachama wa NATO kwa zaidi ya miaka 70, na inajivunia jeshi lake la pili kwa ukubwa.