Ndege ya anga ya kivita isiyo na rubani ya kampuni ya ulinzi ya Uturuki ya Baykar, (UCAV) Bayraktar TB3 ilivunja rekodi ya kupaa juu zaidi kutumia injini iliyotengenezwa Uturuki, na kufikia futi 33,000 katika jaribio la utendakazi.
Kulingana na taarifa kutoka "Baykar Technologies" siku ya Alhamisi, jaribio la Bayraktar TB3 limeendelea kwa mafanikio.
Baada ya kufanya safari yake ya kwanza katika siku ya kuadhimisha miaka 100 ya Jamhuri ya Uturuki tarehe 27 Oktoba 2023, na kufaulu katika majaribio ya utendakazi ya kupaa kwa urefu wa kati na wa juu, Bayraktar TB3 UAV ilikamilisha Jaribio la Utendaji la Mfumo wa Umbali siku ya Alhamisi, na kufikia kiwango cha juu zaidi.
UAV ilikamilisha jaribio hilo kwa mafanikio katika Kituo cha Mafunzo na Majaribio ya Ndege cha AKINCI katika wilaya ya Corlu ya Tekirdag kwa injini ya PD-170 iliyotengenezwa na TUSAS Engine Industries Inc., au TEI.
Rekodi ya kupaa kwa umbali ni ya Bayraktar AKINCI TIHA, ndege ya kivita isiyo na rubani (UAAV) inayopaa futi 45,118 iliyotengenezwa na Baykar.
Kiongozi wa mauzo ya nje katika sekta ya anga
Mnamo Machi 26 mwaka huu, ilifikia hatua nyengine kwa kuruka kwa mafanikio na mfumo wa ASELFLIR-500 uliofanikishwa nchini, unaojulikana kwa utendaji wake bora zaidi duniani.
Ikiwa na mbawa zinazoweza kukunjwa, Bayraktar TB3 itakuwa ndege ya kwanza isiyo na rubani yenye silaha inayoweza kufanya kazi kutoka meli za kivita kama ile ya TCG Anadolu.
Maendeleo haya, pamoja na uwezo wake wa mawasiliano wa hali ya juu, yanachangia mabadiliko makubwa katika sekta ya upelelezi, na misheni ya mashambulizi, ikiboresha kwa kiasi kikubwa uwezo wa ulinzi wa Uturuki.
Kulingana na Jumuiya ya Wasafirishaji nje Uturuki, Baykar, ambayo kwa kiasi kikubwa ilijifadhili, imetegemea mauzo ya nje kwa asilimia 83 ya mapato yake tangu mwaka 2003, na kuongozi sekta ya ulinzi na anga.
Uongozi wa Viwanda vya Ulinzi mnamo 2023 ulitambua mauzo ya nje ya Baykar uliyofikia dola bilioni 1.8 mwaka jana, ikiwa ni zaidi ya asilimia 90 ya mapato yake na theluthi moja ya mauzo ya nje ya sekta hiyo mnamo 2023.
Kama muuzaji mkubwa zaidi wa ndege za kivita sizizo na rubani duniani, Baykar imetimiza asilimia 97.5 ya mikataba yake kupitia mauzo ya nje, na mikataba iliyotiwa saini na jumla ya nchi 34, nchi 33 za Bayraktar TB2 UAV na nchi 9 hadi sasa kwa Bayraktar AKINCI TIHA.