Samuel Eto’o
Mshambuliaji Eto’o kutoka nchini Cameroon ndiye mchezaji wa Afrika aliyetwaa mataji mengi zaidi ya ‘Champions League.’ Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona na Inter Milan ametwaa taji hilo mara tatu; mara mbili na Barcelona mwaka 2005/2006 na mwaka 2008/2009, na taji moja moja akiichezea Inter Milan mwaka 2009/2010. Aidha Eto’o ndiye mfungaji bora kutoka Afrika kwenye ‘Champions League’ akiwa amecheza jumla ya mechi 81.
Didier Drogba
Nyota huyu kutokea Ivory Coast ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi za ‘Champions League’ akiwa na jumla ya mechi 89 huku akimpiku Eto’o kwa idadi ya magoli akiwa na 42. Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Chelsea alishinda UCL na timu hiyo mwaka 2012. Drogba hakupata fursa ya kucheza UCL wakati akiitumika klabu ya Olympique de Marseille ila aliipata fursa hiyo tena akichezea klabu ya Ligi kuu ya Uturuki Galatasaray.
Mohamed Salah
Nyota huyu wa Misri mwenye umri wa miaka 30 amecheza zaidi ya mechi 80 za UCL tangu aanze kucheza soka la kulipwa, huku akiwa ametia kimiyani jumla ya magoli 40 ya UCL akichezea FC Basel, Chelsea, AS Roma na Liverpool. Sasa hivi ndiye mfungaji bora wa UCL kutokea bara la Afrika akiwa tayari amempiku Didier Drogba. Salah amecheza jumla ya fainali tatu za UCL tangu asajaliwe kucheza soka la kulipwa.
Sadio Mane
Mshambuliaji huyu wa Senegal kwa sasa anaichezea klabu ya Bayern Munich ikiwa ndiyo klabu yake ya pili kuchezea kwenye mashindano ya UCL; takwimu zake sio sawa na aliyekuwa mshambuliaji mwenza wake katika klabu ya Liverpool Mohamed Salah. Hatahivyo Mane aling’ara na Liverpool kwenye UCL walipotawazwa Mabingwa mwaka 2019, huku akiwa akifunga magoli manne na kusaidia kufunga(yaani assist) mbili. Mane anashabikiwa sana kwa weledi wake wa kumilika mpira na kutoa pasi zilizokamilika.
Nwankwo Kanu
Mshambuliaji huyu raia wa Nigeria alishinda taji ka UCL mwaka 1995 akichezea klabu ya Ajax Amsterdam. Akiwa amecheza jumla ya mechi 60, nyota huyo vilevile alishida tuzo ya Ballon d’Or ya Afrika mwaka 1996 na 1999. Kwa wachache miongoni mwa vijana wasiomkumbuka, Kanu alikuwa mchezaji mkakamavu aliyefurahisha mashabiki wengi wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa kipindi cha miaka 14.
Riyad Mahrez
Mchezaji huyu raia wa Algeria angali bado kufanikiwa kutwaa taji la UCL. Hatahivyo alikuwa kiungo muhimu katika kuisaidia klabu ya Manchester City kufikia fainali za UCL mwaka 2021, na licha ya kuwa klabu ya Chelsea ilishinda mechi hiyo ya fainali Mahrez alikuwa ni mtaji muhimu kwenye nusu fainali walipowaondoa PSG. Mahrez amechea na wavu mara 17 katika mechi 47 za UCL alizocheza.
Emmanuel Adebayor
Licha ya kuwa nyota huyu raia wa Togo hakutwaa taji la UCL, alifanikiwa kuwakilisha vilabu kubwa barani ulaya ikiwa ni pamoja na; Real Madrid, Arsenal, AS Monaco na Manchester City. Adebayor alitia kimiyani jumla ya magolio 13 ya UCL.
George Weah
Licha ya kuwa mshindi huyu wa Tuzo ya Ballon d’Or mwaka 1995 alikuwa na uzoefu finyu wa UCL kwa kiwango fulani, Weah wakati akiichezea PSG walibanduliwa nje kwenye nusu fainali ya UCL na AC Milan mwaka 1995. Alicheza na wavu mara 14 katika mechi 22 za UCL alizocheza – takwimu zuri zinazostahiki heshima vilevile.
14 Okt 2022
Wachezaji Soka wa Afrika Waliong’ara kwenye Ligi ya Mabingwa wa Ulaya – Champions League
Wachezaji nyota kutokea Afrika Sadio Mane na Mohamed Salah walionesha weledi wao kwenye Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwaka huu. Hii hapa ni orodha ya washambuliaji wa Afrika waliowahi kutikisa UEFA Champions League kwa kishindo.
TRT Français
Habari zinazohusiana
Makala yanayovuma katika kategoria hii
Nini kingine ungependa kujua?
Maarufu