Ligi Kuu NBC imepanda kutoka nafasi ya 6 mwaka 2023 hadi nafasi ya 4 Afrika kwa mwaka 2024./Picha: Wengine

Ligi Kuu ya soka nchini Tanzania (NBC Premier League) imeshika nafasi ya nne kwa ubora wa soka barani Afrika.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS), ligi ya NBC imekusanya jumla ya alama 266,75 na kushika nafasi ya 57 duniani ikiwa imezipita Ligi Kuu za nchini Nigeria, Kenya, Afrika Kusini, Ivory Coast, Ghana, Angola, Tunisia na Uganda.

NBC imepanda kutoka nafasi ya 6 mwaka 2023 hadi nafasi ya 4 Afrika kwa mwaka 2024, ikiashiria kuongezeka kwa ushindani na ubora wa ligi hiyo kimataifa

NBC Premier League huhusisha jumla ya timu 16 ambapo bingwa wa ligi hiyo pamoja na mshindi wa pili watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika huku ile ya tatu ikishirikisho Kombe la Shirikisho.

TRT Afrika